19 April 2012

Hivi maisha ni nini jamani!

Jana nikiwa na baadhi ya jamaa zangu tukijaribuu kuangalia jinsi ya kufanya ili uweza kutoka kimaisha, Kwa kweli tulizungumza mambo mbalimbali ya kujenga maisha yetu ya baadae,
Mpenzi msomaji wangu leo nataka nikupatie moja ya yale amabayo tulikuwa tukiyajadilii pamoja na kuyatafutia njia zake, Mazungumzo yet yalichukua takribani mda wa masaa mawili na nusu kila mtu akitoa la kwake alilonalo moyoni mwake,

Msomaji wangu nisikulaze huko bali moja kwa moja nikuambie kuwa kitu ambacho kilionekana kuleta mjadala mrefu na hatimaye sote tukawa kwenye usawa ni , je uwongo waweza kumsaidia mtu kushinda kitu fulani maishani mwake au ?

Msomaji wangu ni kwamba  tulikuwa tunajaribu kuongea kwa mifano iliyo hai mingi, mmoja ambaye alionekana kutetea hoja hii tanagu mwanzo Aliweka wazi kuwa yeye tangu akiwa darasa la saba akiota sana na kupenda sana kuwa mwandishi wa habari japo kuwa hakupenda kuwambia wazazi wao,  Alipoendelea na masomo na hatimaye akamaliza kidato cha nne , akachanguliwa na kujiunga na kidato cha tano katika sekondali ya Uyui, Alipomaliza kidato cha sita alistahili kwenda chuo cha Ualimu, Lakini anasema wazazi wake walipokuwa wanajiandaa kumpeleka chuoni akawa amevunja ukimya na kuwambia kuwa Ualimu sio ndoto yangu, akasema ndoto yanaga ya mda mrefu ni Uhandishi wa habari, Wazazi wakatupilia madai yake ya kumtaka awe mwandishi, Anasema kuwa akalia pamoja na kuomba lakini huku wazazi wakiendelea kukataa, Walipokataa mawazo yake akaona kuwa sasa sina jinsi kilichopo ni kutafuta uwongo mtakatifu , huku akisema kkuwa endapo mambo yatakuwa yameharibika heri kujilaumu kuliko kuwalaumu wazazi wangu,

Akwawambia kuwa mama, na baba tayari nimefuta mawazo niliyokuwa nayo na kuwambia kuwa sasa niiko tayari kujiunga na chuo cha ualimu, Lakini kijana huyo alikuwa ameshajua fika kuwa chuoni hapa kuna pia faculty ya uhandishi alipowambia wakasema...............................................itaendelea mpenzi msomjaji wangu

No comments: