15 April 2012

MPANGO WA KITUO CHA REDIO CHA FADECO FM KUWABAINI WALEMAVU ZAANZA KUZAA MATUNDA

Siku chache baada ya redio fadeco na jopo la utafiti kuwasilisha taarifa ya walemavu waliobainiwa vijijini na changamoto wanazokabiliana nazo waziri wa afya na ustawi wa jamii Haji Husein Mponda amewahasa walemavu wote nchini kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni ya kuandikwa kwa katiba mpya.

Mh Haji amesema kuwa mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa katiba mya unawahusisha watanzania wote pasipo kujali dini, kabila na uwezo wa mtu mambo ambayo yanawafanya watanzania waliowengi kutoshiriki katika kutoa maamuzi katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Ameongeza kuwa walemavu hawana tofauti na watu wengine waokwenda kutoa maoni hivyo kusisitiza kuwa ni jukumu na nafasi ya kila mtu kushiriki kikamilifu.

Zoezi hili la redio fadeco kuwabaini walemavu wilayani karagwe limefanikiwa baada ya shirika la CCBRT kutangaza kuwatibu akina mamma wanaosumbuliwa na fistula bila gharama yoyote na mdomo wazi kwa watoto wadogo maana ya chini ya miaka mitano.

Pia wadau mbalimbali wanaotetea haki za wanyonge na kupiga vita vitendo vya unyanyasaji wamejitokeza kuwasaidia walemavu kwa kile kitakachowezekana kusaidia.

Zoezi hili linatazamiwa kufanyika mkoa mzima wa kagera kwa kuanza na wilaya mojamoja ambapo maandalizi yatakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa na chombo hiki.

No comments: