16 April 2012

http://www.g5click.com/music/playlist/popup?playlistUrl=http%3A//www.g5click.com/music/

15 April 2012

USIOMBE IKAKUKUTA HII

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA TEMBO!! Mkazi wa kijiji cha Ibebu kata ya Mwangudo wilayani Meatu Mkoani Simiyu nchini Tanzania Ibese Doto (40) amefariki dunia baada ya kukanyagwa na Tembo akiwa shambani kwake akilinda mazao yake yasiharibiwe na ndege na wanyama. Kaimu kamanda wa polisi Mkoani Shinyanga amewaambia waandishi wa habari kuwa marehemu huyo akiwa shambani kwake mara ghafla alitokea Tembo huyo na kuanza kumshambulia na baadaye kumkanyaga hadi kuuuwa. Kaimu kamanda huyo amesema kundi kubwa la Tembo limevamia katika kitongoji hicho likitokea kwenye hifadhi ya akiba ya pori la Maswa hali aliyodai inahatarisha maisha ya wananchi. Amesema jeshi la polisi mkoani humo bado linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na namna gann ya kuweza kakabiliana kundi hilo kubwa la Tembo waliovamia katika maeneo hayo na hivyo kuwataka wananchi kujihadhari nao.

TUJIULIZE WENYEWE KWANZA


MASWALI YA KUJIULIZA WEWE MWENYEWE BINAFSI

Muda mwingi huwa tunapenda kuwauliza watu wengine maswali.Lakini mimi nitakuwa nakuletea maswalimatano yakujiuliza wewe mwenyewe binafsi.
1.Wewe ni nani?
2.Unajipenda?kama ndio kwa nini kama sio kwa nini?
3.Ni vitu gani muhimu katika maisha yako?
4.Ni mafanikio gani unayojivunia katika maisha yako kwa sasa?
5.Nini lengo lako duniani?kwa nini upo duniani?

Kwa leo maswali matano ni hayo na nitakuwa nakuwekea mara kwa mara.Sio lazima unijibu mimi,jijibu wewe mwenyewe ila unaweza kushare nami kunifahamisha kama umeguswa.

NOTE:Kama ni mtu wa kuchukua mambo kirahisi bila kufikiri kwa kina unaweza kuhisi ni maswali yasiyo na maana.Ila ni maswali makubwa sana unayotakiwa kujiuliza.

KANUUMBA UMEACHA SIMANZI KUMBWA KWA WATANZANIA


TASWIRA MBALI MBALI ZA KUAGWA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Eneo katika makaburi ya kinondoni ambapo mwili wa marehemu Steven Kanumba unapumzishwa.
Polisi wa usalama barabarani na kazi ya ziada.
Watu walivyofurika kwa wingi.
Wengine juu ya miti.
Wasanii mbalimbali waliubeba mwili wa marehemu kutoka kwenye gari kuelekea sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuagia.

MWILI WA KANUMBA WAAGWA PALE LEADERS CLUBNA KUZIKWA LEO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

Picha kwa hisani ya dj choka.

MPANGO WA KITUO CHA REDIO CHA FADECO FM KUWABAINI WALEMAVU ZAANZA KUZAA MATUNDA

Siku chache baada ya redio fadeco na jopo la utafiti kuwasilisha taarifa ya walemavu waliobainiwa vijijini na changamoto wanazokabiliana nazo waziri wa afya na ustawi wa jamii Haji Husein Mponda amewahasa walemavu wote nchini kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni ya kuandikwa kwa katiba mpya.

Mh Haji amesema kuwa mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa katiba mya unawahusisha watanzania wote pasipo kujali dini, kabila na uwezo wa mtu mambo ambayo yanawafanya watanzania waliowengi kutoshiriki katika kutoa maamuzi katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Ameongeza kuwa walemavu hawana tofauti na watu wengine waokwenda kutoa maoni hivyo kusisitiza kuwa ni jukumu na nafasi ya kila mtu kushiriki kikamilifu.

Zoezi hili la redio fadeco kuwabaini walemavu wilayani karagwe limefanikiwa baada ya shirika la CCBRT kutangaza kuwatibu akina mamma wanaosumbuliwa na fistula bila gharama yoyote na mdomo wazi kwa watoto wadogo maana ya chini ya miaka mitano.

Pia wadau mbalimbali wanaotetea haki za wanyonge na kupiga vita vitendo vya unyanyasaji wamejitokeza kuwasaidia walemavu kwa kile kitakachowezekana kusaidia.

Zoezi hili linatazamiwa kufanyika mkoa mzima wa kagera kwa kuanza na wilaya mojamoja ambapo maandalizi yatakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa na chombo hiki.